top of page

MTU AANDAE SHINDANO LA KUPIKA SHILOLE AKINISHINDA NAMPA KISA ANIKATE MIKONO - ESHA BUHETI

Mambo ni mazito imefika hatua sasa Esha Buheti na Shilole wawekwe chini wayamalize tu.

Baada ya jana Shilole kufunguka kuwa Esha Buheti anatuma watu wamtukane kwamba kapendelewa tuzo ila hakustahili bali alistahili Esha ambapo Shilole alikazia kwamba Esha abadilike aache wivu ili afanikiwe hatimaye Esha leo amejibu mapigo ambapo amesema haya



baada ya kuulizwa kati yako na Shilole nani anajua kupika?

"Swali gani la kitoto hilo? Ngoja nikwambie huwezi kunishindanisha mimi na Shilole hata yeye mwenyewe anajua mimi napika kila kitu sitegemei wapishi"

"Wapishi wengi wanaokuja kwangu wanakuwa hawajui kupika nawatrain mimi mwenyewe na hili swali sitaki mimi kulijibu natamani atokee mtu aandae mpambano wa watu hawa wawili bila msaidizi nina kuapia Shilole akinishinda kupika kwenye hilo tangazo nampa kisu anikate mikono sitopika tena Shilole amenishinda"


Kwako mdau unahisi nani hapa ni noma kwa mwenzake?

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page