
Na Ester Madeghe,
Aliyekuwa kamanda wa Lord's Resistance Army (LRA) Thomas Kwoyelo amehukumiwa kutumikia adhabu ya miaka 40 jela kwa makosa ya uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Thomas Kwoyelo amesema alitekwa nyara na kugeuzwa kuwa mwanajeshi wa kundi hilo akiwa na umri wa miaka 12 lilokuwa linafanya harakati zake kaskazini mwa Uganda na katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC) Kitengo cha Kimataifa cha uhalifu katika mahakama kuu ya Uganda kilitoa hukumu ndefu kwa Thomas Kwoyelo katika kesi ya kwanza ya aina yake nchini humo.
Thomas Kwoyelo anashtakiwa kwa makosa 44 kati ya 78, ambayo ni pamoja na mauaji, ubakaji, utekaji nyara na unyang'anyi, ambapo amehukumiwa hukumu nyingi kuanzia miaka mitano hadi 40, kwa wakati mmoja.
Kamanda huyo wa zamani wa LRA alikuwa anakabiliwa na kifungo cha maisha au adhabu ya kifo lakini majaji wamesema amekumbwa na yote mawili kwa sababu alikuwa ameajiriwa kama mtoto katika kundi la waasi.
Majaji hao wameongeza kuwa, Thomas Kwoyelo ameonyesha majuto na ameonekana kuwa si tishio tena kwa jamii. Hukumu yake itapunguzwa kwa miaka kumi na tano ambayo tayari ametumikia katika kifungo cha miaka 15.
Hata hivyo Mawakili wake wamesema kuwa wanapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu ya mteja wao. Jeshi la Lord's Resistance Army linashutumiwa kwa kutekeleza mauaji kaskazini mwa Uganda tangu kuanzishwa kwake mwishoni mwa miaka ya 1980 na Joseph Kony.
Comments