top of page

MUIMBAJI WA ZABRON SINGERS MARCO JOSEPH AFARIKI DUNIA

Taarifa tulizopokea asubuhi zinaeleza kuwa Kiongozi @japhetzabron_official wa Kundi maarufu na kongwe la Muziki wa Injili hapa Nyumbani Tanzania @zabronsingers amethibitisha taarifa ya kufariki Dunia kwa moja kati ya kiongozi wa kundi hilo ndugu Marko Joseph ambaye pia alikuwa ni muimbaji.





Akizungumza na Chomoza Media leo @japhetzabron_official amesema sababu zilizopelekea kifo cha mpendwa wetu Marko Joseph ni maradhi ya Moyo. Ambayo alianza kuumwa siku chache kabla ya kufikwa na umauti.


Jitihada za kutibia tatizo hilo kwa mpendwa wetu zilianzia hospitali ya Bugando mwanza na baadae alipewa uhamisho kuelekea hospitali Moi hapa Dar. Msasa Media tunatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwa Msiba huu Mzito. Tunaomba faraja kuu iwe nanyi @zabronsingers pamoja na kiongozi @japhetzabron_official


Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.



Source: Chomoza Media

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page