top of page

MUONEKANO WA KOMBE LA CRDB BANK FEDERATION CUP JE NI NANI ATABEBA KATI YA AZAM VS YANGA?

Huu ndio muonekano wa Kombe la CRDB BANK FEDERATION CUP litakoletolewa kwa


mshindi wa fainali hizo mwishoni mwa juma hili siku ya Jumapili ya Juni 2 mwaka huu Azam FC akipambana na Yanga SC huko Visiwani Zanzibar kupitia ukurasa wa Instagram wa wadhamini wakuu wa mashindano hayo Benki ya CRDB wamepost Kombe hilo na kuandika

"Macho hayachoki kukutazama Baada ya kushuka kutoka Mlima Kilimanjaro akiwa na tu alama twa volcano, ulinzi wa pembe adhimu za ndovu na ulimbwende wa dhahabu za Geita, mwana mwali KOMBE alitua mjengoni na kujinafasi kwenye kila kona kwa picha za mpwito mpwito

Kelele tatu kwa kombe lakeeeee"

Je nani atalibeba?

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page