top of page

MUUZA DAWA MKUBWA WA UHOLANZI ATIMUKIA SIERRA LEONE, YADAIWA KUWA ANALINDWA NA SERIKALI

Na VENANCE JOHN


Wizara ya habari nchini Sierra Leone jana imesema kuwa inachunguza ripoti za vyombo vya habari kwamba mfalme wa Ulaya wa kuuza dawa za kulevya aina ya cocaine, Bw. Jos Leijdekkers yuko nchini Sierra Leone na kwamba anapewa ulinzi wa hali ya juu nchini humo.


Vyanzo viwili vimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba Leijdekkers, ambaye mwezi Juni mwaka jana alihukumiwa bila kuwepo mahakamani kwa miaka 24 jela na mahakama ya Uholanzi kwa kusafirisha zaidi ya tani 7 za kokeini, alikuwa nchini Sierra Leone tangu mwanzoni mwa 2023.


Msemaji wa ofisi ya waendesha mashitaka wa Uholanzi alisema kwamba Leijdekkers amekuwa akiishi Sierra Leone kwa angalau miezi sita Leijdekkers yuko kwenye orodha ya polisi wa Ulaya (Europol) ya watu waliotoroka ambao wanasakwa sana.


Katika taarifa yake, wizara ya Sierra Leone imesema polisi wa nchi hiyo wako tayari kushirikiana na serikali ya Uholanzi, Interpol na vyombo vingine vya kimataifa vya kutekeleza sheria kuhusu kesi hiyo.


Video na picha zilizothibitishwa na shirika la habari la Reuters za Misa ya kanisa huko Sierra Leone mwezi Januari tarehe 1, 2025 zinamuonyesha Leijdekkers mwenyewe umri wa miaka 33, akiwa ameketi safu mbili nyuma ya Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio.


Katika picha hizo, Leijdekkers alikuwa amekaa karibu na mwanamke ambaye vyanzo vitatu vilisema alikuwa binti wa rais wa nchi hiyo Julias Maada Bio, Bi Agnes na ambaye walisema alikuwa ameolewa na Leijdekkers.


Vyanzo vitatu vililiambia shirika la habari la Reuters kwamba Leijdekkers ananufaika na ulinzi wa hali ya juu nchini Sierra Leone, ambayo maafisa wa sheria wa kimataifa wanasema ni sehemu ya kupitisha kiasi kikubwa cha kokeini za Amerika Kusini zinazoelekea Ulaya.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page