top of page

MWAKINYO ASEMA ANAJUTIA KUPOTEZA USINGIZI WAKE KUTAZAMA PAMBANO LA KIDUKU...

Bondia Hassan Mwakinyo ameamua kutoa ya Moyoni juu ya kilichofanyika usiku wa jana ambapo kulikuwa na Pambano la ngumi la bondia Twaha Kiduku aliyeibuka na ushindi wa TKO



kwenye mzunguko wa tano dhidi ya bondia kutoka India Harpreet Singh ambapo Mwakinyo ametoa maoni yake akidai kwamba Kiduku anatafuta mabondia wa kuja kuachia sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka haya "Najutia usingizi wangu, yaani leo umeonyesha kuwa wewe hauna sifa wala vigezo vya kuwa pro, nimekua kwenye boxing kwa takribani miaka 17 sasa hakuna ushindi wa namna ile, Kibenju nertwork ya mlundwa imekubeba sana kutafuta bondia wa kuja kuachia na hii ndio salama yako." "Kama sio ofa na jamaa angeamua kukaza angekuvua nguo tena, kiwango chako ni kibovu sana, siku hadi siku haukui ki-mchezo, Simba na Yanga zinafuzu kila siku na zinabadilisha walimu wewe unapigwa kila siku lakini ni kama umefunga nae ndoa."

"Listen ukitaka kujilinganisha sawa na mtu kwa ubora make sure baadhi ya vitu mnafanana au unakuwa zaidi yake." Mwakinyo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page