top of page

MWALIMU ATUPWA JELA MIAKA 30 BAADA YA KULAWITIWA NA MWANAFUNZI WAKE, ALIMRUBUNI..




Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Ramadhani Nanyalika amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema mwalimu huyo siku za nyuma alijenga urafiki shuleni na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa shuleni na kumtaka akamtembelee nyumbani.

Amesema mwalimu huyo alimtaka mwanafunzi huyo akamtembelee nyumbani na alipoenda alianza kumuonyesha video chafu kupitia simu janja na baadae kumtaka amuingilie kinyume na maumbile. Baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho ndipo mwalimu akaanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule.

Baada ya vitisho hivyo mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake.

Katika hatua nyingine Bakari Katembe mwenye umri miaka 19 mkazi wa Kijiji cha Mdumbwe amehukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu.

Mtuhumiwa huyo alimlaghai mtoto huyo kwa kumununulia pipi kisha kumchukua kwenda naye nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page