top of page

MWANADADA MTANZANIA CLARALUVANGA

AIPA UBINGWA TIMU YA RONALDO UPANDE WA WANAWAKE

Fahamu kuwa Mshambuliaji wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia upande wa Wanawake



@claraluvanga14 amekuwa miongoni mwa nyota ndani ya kikosi hicho waliosaidia kuibuka na ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo.

Clara ambaye ni nyota wa zamani wa Yanga Princess alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Al Hilal

Ikumbukwe kuwa klabu hiyo ya Al Nassr ndiyo timu ambayo anaichezea nyota wa zamani wa timu za Juventus, Real Madrid, Manchester United na timu ya taifa Ureno, Cristiano Ronaldo CR7 ambapo kwa upande wao wanaume mambo bado yanasuasua kwani wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi nyuma ya Al Hilal kwa alama 9.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page