top of page

MWANAHARAKATI SWEDEN ANAYEPINGA UISLAMU AULIWA KWA KUPIGWA RISASI, WATANO WAKAMATWA

Na VENANCE JOHN


Polisi wa nchini Sweden wamewakamata watu watano leo baada ya mwanaharakati wa kupinga Uislamu Salwan Momika kutoka nchini Iraq kuuawa kwa kupigwa risasi saa chache kabla ya hukumu ya mahakama kutolewa katika kesi yake ya kuchoma Qur'an. Waziri mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson ameeleza wasiwasi wake juu ya uhusiano wa mauaji hayo na mataifa ya kigeni.


"Ninaweza kuwahakikishia kwamba huduma za usalama zinahusika sana kwa sababu ni wazi kuna hatari kwamba kuna uhusiano na nguvu ya kigeni," Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson amesema katika mkutano na waandishi habari leo. Watano hao walikamatwa kuhusiana na kupigwa risasi kwa Salwan Momika, mwenye umri wa miaka 38, mkimbizi wa Iraq, katika nyumba moja mjini Sodertalje karibu na Stockholm hapo jana.


Hata hivyo polisi hawakusema ikiwa mshambuliaji ni miongoni mwa watano hao waliokamatwa. Momika alichoma na kunajisi nakala za Qur'an hadharani, kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu mwaka 2023.


Mahakama ya Stockholm ilitakiwa kumhukumu Momika na mwanamume mwingine siku ya leo Alhamisi katika kesi ya jinai kwa makosa ya uchochezi dhidi ya kabila au taifa, kuhusiana na uchomaji moto wa Qur'an lakini ikaahirisha hukumu hiyo. Kuchoma Qur'ani kunaonwa na Waislamu kama kitendo cha kufuru kwa sababu wanalichukulia kuwa neno halisi la Mungu.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page