top of page

MWANAMKE ALIEOLEWA NA WAUME WAWILI, ATAKA KUOLEWA NA MUME WA TATU.

Imekua gumzo mtandaoni baada ya Kenya Stevens, mwanamke wa Marekani ambaye ana ndoa ya polygamy (Ndoa ya mume zaidi ya mmoja) akiwa na waume wawili, Carl na Tiger, ameonesha nia yake ya kupata mume wa tatu.



Kupitia kipindi cha TLC kinachoitwa Seeking Brother Husband, Kenya alielezea jinsi yeye na waume wake wawili wanavyoishi pamoja kwenye nyumba moja. "Nimeolewa na mume wangu wa kwanza, Carl, kwa miaka 26 na mume wangu wa pili, Tiger, kwa miaka tisa," alisema Kenya.


Kenya anaamini kwamba wanawake wanapaswa kuwa na uhuru sawa na wanaume kuwa na wapenzi wengi. Aliongeza kwa kusema kuwa anaendelea kuingia kwenye uhusuiano mpya huku bado akiwa pamoja na waume wake wawili, akisema kwamba anapenda upendo na anafurahia maisha hayo.


Akieleza maisha yake na waume wake wote wawili huko North Carolina, Kenya alisema, "Nina wapenzi na mawasiliano mengi. Poligamiya si kwa kila mtu, kwani inaweza kuwa ngumu katika jamii ambapo uhusiano wa mmoja mmoja ndio kawaida."


Safari yake ya poligamiya ilianza alipompenda mwanaume mwingine na kuzungumza hisia zake na Carl, mume wake wa kwanza. Ingawa ilimchukua Carl miaka miwili kukubali wazo hilo, hatimaye alikubali, akisema, "Unapaswa kuwapa wanawake nafasi ya kujieleza."


Tiger, mume wake wa pili, alieleza wasiwasi wake kuhusu tamaa ya Kenya ya kupata mume wa tatu, akisema, "Je, hatutoshi? Nina wasiwasi kwamba mwanaume mwingine huenda akanishinda kwa njia fulani." Licha ya changamoto hizi, familia inaendelea kusimamia uhusiano wao wa kipekee.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page