top of page

MWANASIASA MKONGWE NCHINI UGANDA DR. KIZA BESIGYE AGOMA KULA GEREZANI

Na VENANCE JOHN


Kiongozi wa upinzani wa Uganda Dr. Kizza Besigye, amesusia kula katika gereza la Luzira mjini Kampala.


Wasaidizi wake wanasema Besigye analalamikia kuendelea kushikiliwa licha ya uamuzi wa mahakama kuu ya nchi hiyo mwezi uliopita kuzuia mahakama za kijeshi kuwahukumu raia. Harold Kaija, msaidizi wa kisiasa wa chama cha Besigye cha People’s Front for Freedom (PFF), amethibitisha hatua ya kiongozi huyo kususia kula.


Besigye, aliyekuwa daktari wa kibinafsi wa Rais Yoweri Museveni, alikamatwa katika mazingira ya kutatanisha mwezi Novemba mwaka jana jijini Nairobi nchini Kenya pamoja na msaidizi wake wa kisiasa, Obeid Lutale. Wawili hao baadaye walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Kampala, ambapo walishtakiwa kwa kumiliki silaha na risasi kinyume cha sharia mashtaka ambayo wanapinga.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page