Na VENANCE JOHN
Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Uganda Dr.Kizza Besigye, aliyegoma kula kwa wiki moja, amerudishwa gerezani baada ya kuwa katika matibabu katika kliniki ya afya usiku kucha. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 68 alikimbizwa katika kituo cha matibabu cha kibinafsi katika gari la wagonjwa la gereza huku afya yake ikizidi kuzorota, wakili wake Erias Lukwago aliandika mapema kwenye mtandao wa Facebook.

Besigye alishtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria, kutishia usalama wa taifa, pamoja na uhaini, kosa ambalo akikutwa na hatia hukumu yake ni ya kifo. Hata hivyo Dr. Besigye anakanusha tuhuma hizo.
Habari kuhusu afya yake zilikuja saa chache baada ya waziri wa baraza la mawaziri kusema kuwa amemtembelea Besigye jela na kumtaka aanze kula huku akiahidi kufuta kesi yake ya kijeshi.
Mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amewania urais dhidi ya kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni mara nne, amekuwa kizuizini tangu alipotekwa nyara nchini Kenya mwezi Novemba na kurudishwa Uganda kujibu mashtaka ya kijeshi.
Commenti