top of page

MWANASIMBA MWENYE MAPENZI NA KLABU ATAKUWA AMEMUELEWA M/KITI MANGUNGU - AHMED ALLY

Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya

"Nimemsikiliza kwa makini sana Mwenyekiti wetu Murtaza Mangungu kwenye mahojiano yake na Clouds Fm, itoshe kusema tu Mwana Simba mwenye mapenzi na klabu yake atakua amemuelewa vema Mwenyekiti.

Mwenyekiti ametolea ufafanuzi mambo mengi ya msingi kuhusu timu yetu lakini kubwa ni kwamba hakuna tofauti yeyote baina yake na Mwekezaji Mohammed Dewji na yeye akiwa Mwenyekiti wa Simba anamuunga mkono Dewji na anamuheshimu na kumpongeza kwa kujitoa kwake katika klabu yetu na ataendelea kumpa ushirikiano kwa maslahi ya Simba Sports



Club..

Ameongeza kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni Mohammed Dewji kuteua Wajumbe wa Bodi kuziba nafasi ya wale waliojiuzulu kisha wakae kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kujadili mustakabali wa timu yetu.

Kuhusu Usajili Mwenyekiti Mangungu amesema tayari wameshapokea taarifa ya Benchi la ufundi la wameshafanya tathimini hivyo kikao cha Bodi ya wakurugenzi kitaamua zaidi.

Akihitimisha mahojiano yake kwa kuwataka Wana Simba kuwa watulivu huku akisema GIZA HALIONDOLEWI NA GIZA bali giza huondolewa na Mwangaza..

"Mtazamo wangu" Tumemsikia Mwenyekiti aliyejiuzulu Salim Abdallah, Tumemsikia Mwekezaji Mohammed Dewji na tumemsikia Mwenyekiti Murtaza Mangungu wote wamesisitiza Umoja na Utulivu"

Wana Simba tutulie na tuwape ushirikiano viongozi wetu wapate utulivu wa kuisuka Simba mpya tunayoitaka.

Pia kumekua na Nukuu nyingi Fake za Mwenyekiti wetu Murtaza Mangungu zenye lengo la kumgombanisha na Mashabiki niwaombe Wana Simba tuachanae na taarifa hizo

Simba mpya inakuja na Simba imara inarejea". Ahmed Ally.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page