top of page

MWANAUME ALIYETIMULIWA NA MWANAMKE

MAHAKAMA YAAMURU NAE APATE MALI ZA MWANAMKE HUYO...

Mwanaume mmoja, mkazi wa Nairobi, Kenya ambaye alitimuliwa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye kama kimada kwa miaka 25, sasa atakuwa anapata asilimia 30 ya mali waliochuma na mwanamke huyo kipindi wakiwa pamoja.



Mwanaume huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, atakuwa anatia kibindoni kodi ya wapangaji 11 kati ya 38 katika nyumba za makazi na fremu za biashara zinazomilikiwa na mwanamke huyo na pia atafidiwa kiasi alichonyimwa na mwanamke huyo tangu mwaka 2011 alipomtupia virago nje.

Jaji wa mahakama kuu alikubaliana na hukumu ya awali katika kesi hiyo iliyotolewa na mahakama ya chini kwamba, ingawa wawili hao hawakuwa na ndoa rasmi, lakini mwanaume huyo alishiriki kuchuma mali hizo na mpenzi wake huyo na hivyo anatakiwa kupata asilimia 30 ya mali hizo.

Tumezoea kuona mambo haya kwa wanawake ndio wakitaka nao wanufaike na mali za wanaume walizochuma pamoja.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page