top of page

MWANDISHI WA HABARI JOSEPHINI KIBIRITI AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Aliyekuwa Mwakilishi wa StarTV mkoani Lindi Josephine Kibiriti amefariki Dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2024.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi



Protas Mutayoba ajali hiyo imetokea eneo la Nyamwage mkoani Pwani baada ya gari waliyokuwa wakisafiria Waandishi hao kugongana na Lori.

Kamanda Mutayoba ameongeza kuwa ajali hiyo pia imesababisha kifo Mwandishi wa Channel Ten Abdallah Nanda.

Waandishi wa Habari hao walikuwa wanatokea jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo wakielekea mkoani Lindi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page