Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Adolf Mkenda amesema
"Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara imepanga kutekeleza
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_d4ef47af72d14a6bbfb483952078c334~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_d4ef47af72d14a6bbfb483952078c334~mv2.jpg)
vipaumbele vitano vyenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kuwezesha vijana wa Kitanzania kupata maarifa, ujuzi, kujiamini, kujiajiri na kuajirika. Vilevile, vipaumbele vyenye kujielekeza katika kutegemeza tafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu katika agenda ya maendeleo ya nchi.
"Mheshimiwa Spika, vipaumbele vya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni kama vifuatavyo:
kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini;
kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu);
kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu;
kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu; na
kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu."
Comments