Na Ester Madeghe,
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Mipaka nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Kaka yake Daniel Chebukati amethibitisha kufariki kwake akiwa na miaka 63. Bosi huyo wa zamani wa IEBC alikuwa amelazwa hospitalini akipokea matibabu kwa wiki nzima. Mpaka sasa ugonjwa uliomuondoa maisha yake haujawekwa wazi.
Chebukati alihudumu kama mwenyekiti wa Tume ya IEBC kwa miaka sita kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2023. Alikuwa wakili mwenye uzoefu wa miaka 37 na alisimamia ofisi yake binafsi ya sheria kwa kipindi cha miaka 20.
Alikuwa na utaalamu katika tasnia ya sheria za biashara, sheria za makampuni, usimamizi wa makampuni, na utatuzi wa migogoro. Pia, alikuwa mwanasiasa na mshirika wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), ambacho alijiuzulu kabla ya kuomba nafasi ya Mwenyekiti wa IEBC.
Comments