top of page

MWIGIZAJI VEE AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, JE NI WA AZIZ KI?

Mwigizaji wa Bongo Movie Vanessa Kashera ameweka wazi kujifungua mtoto wa kiume kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo mastaa mbalimbali wamempongeza ambapo katika video tuliyoina Msasa wachezaji Pacome na Yao Yao walikuwa hospitali wabembeba mtoto huyo wakitoa pongezi.


Mwanadada huyu ambaye amekuwa akitajwa kuwa kwenye mahusiano na mchezaji wa Yanga SC Mburkinabe Aziz Ki ameandika haya kupitia ukurasa wake huo


"Moyo wangu umejaa furaha na kinywa changu kimejaa sifa. Ulinipeleka katika safari hii salama na kuamuru hatua zangu kulingana na neno lako. Asante Mungu kwa bando la furaha yangu. Haikuwa rahisi kwangu Lakini Bwana ulinifanyia.




Sura hii inaitwa MUNGU ALIFANYA!!!


Mpendwa MWANANGU


ASANTE kwa kunikaribisha kuwa mama, unafanya yote yafaa Nataka kutumia maisha yangu yote kuwa mama yako. Na nataka ukue ukijua kuwa pasipo MUNGU wewe si kitu sio Mungu wala si chochote Mfalme wangu mdogo Ninapoanza safari hii mpya na wewe, naomba uyajaze maisha yangu na furaha tupu Nakupenda sana Mtoto wangu wa kiume


Kwa kila mwanamke anayetafuta zawadi ya mtoto, ninaomba kwamba Bwana akujibu upesi na akubariki sana katika jina la Yesu. (Hakika mtashuhudia wema wa Mungu.)." Swali lililobaki je mtoto huyu ni wa Aziz Ki? Ambaye kwa sasa anatamba na Hamisa Mobetto! Wanasema damu nzito kuliko maji wacha tusubiri tutajua tu ukweli.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page