Na VENANCE JOHN
Chombo cha anga za juu cha cha Marekani NASA kilichotengenezwa kinajaribu kuweka historia kwa kukaribia zaidi kwenye jua. Kifaa hicho kitakuwa kinakwenda kwa kasi zaidi kuliko kitu chochote kilichoundwa na binadamu, kwani kitakuwa na kasi ya 430,000 Mph, sawa na kuruka kutoka London hadi New York chini ya sekunde 30.

Chombo cha Parker Solar Probe kitatumika kuingia katika anga hewa ya nje ya sayari ya dunia yetu ambayo inazunguka jua kwa kitaalam hewa hiyo inaitwa CORONA, ambapo kifaa hicho kitastahimili halijoto kali na mionzi mikali ya jua.
Mbele ya kifaa hicho kinalindwa na ngao yenye unene wa 11.5cm (inchi 4.5) yenye mchanganyiko wa kaboni lakini mbinu ya chombo hicho ni kuingia na kutoka kwa haraka kwenye angahewa ya jua inayojulikana kama CORONA.
Dr. Nicola Fox, mkuu wa sayansi kutoka NASA, anasema; "kwa karne nyingi, watu wamejifunza jua, lakini hupati uzoefu wa mazingira ya mahali hadi utalitembelea, na kwa hivyo hatuwezi kuona anga ya nyota yetu isipokuwa tukipitia."
Kifaa cha Parker Solar Probe kilizinduliwa mwaka 2018, kuelekea katikati mwa mfumo wa jua. Tayari kifaa hicho kimepita jua mara 21, kikikaribia zaidi, lakini kwa mara hii wakati watu wakiwa kwenye mkesha wa krismasi awamu hii itakuwa ni ya kuvunja rekodi.
Nicola Fox wa NASA anasema: "tuko maili milioni 93 kutoka kwenye jua, kwa hivyo nikiweka jua na dunia umbali wa mita moja, kifaa cha Parker Solar Probe kiko sentimita nne kutoka kwenye jua, kwa hiyo ni karibu." Uchunguzi utalazimika kustahimili halijoto ya 1,400c na mionzi ambayo inaweza kufifisha kielektroniki cha ndani.
Comments