top of page
Radio on air

NASHAURI VILABU VYA MPIRA WALETE WACHEZAJI TUWAFANYIE CHECK UP KABLA YA USAJILI - PROF. JANABI


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema vilabu vikubwa vya Tanzania (Simba, Yanga, Azam na vingine) vinafanya usajili wa wachezaji kwa gharama kubwa kutoka nje na wa ndani lakini huwa havijui vyema hali za kiafya za wachezaji hao.

"Tungewashauri sana kabla hawajasaini mikataba, hebu naomba waje Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila wafanyiwe check up. Manake unamnunua mchezaji kwa dola laki moja, laki moja na nusu, dola laki mbili halafu anacheza mechi mbili baada ya hapo hachezi tena. Sihitaji kutoa mifano, najua kuna moja ya klabu yetu kubwa imemsajili mchezaji mpaka leo hajacheza. Amecheza mechi mbili nafikiri kama sio tatu. Sasa tusiingie kwenye hizo gharama. Kitu cha kwanza nafikiri akishapatikana mchezaji aje apate, tunasema clean bill of health kabla hamjatia saini ya

mwisho," amesema Professa Janabi.

Profesa Janabi ameyasema hayo leo Juni 10, 2024 alipozungumza na vyombo vya habari katika Hospitali la Taifa ya Muhimbili-Mloganzila ambapo aliongozana na mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upandikizaji wa nyonga na magoti bandia katika Hospitali ya Mloganzila ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara, Mzee Sunday Manara.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page