Na VENANCE JOHN
Maafisa kutoka nchi za Algeria, Nigeria na Niger wametia saini mikataba mipya inayolenga kuharakisha uendelezaji wa bomba kubwa la gesi asilia ambalo likuwa linapeleka gesi asilia bara la Ulaya.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_16d3c6b72a794fe497ab4e4e767d170e~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_16d3c6b72a794fe497ab4e4e767d170e~mv2.jpeg)
Bomba hilo la gesi ambalo lililotangazwa mwaka 2009, litasafirisha mabilioni ya mita za ujazo za gesi kutoka Nigeria kupitia Niger hadi Algeria. Kutoka hapo gesi hiyo itaweza kusafirishwa kupitia bomba la chini ya bahari kwenda Italia, au kupakiwa kwenye meli za gesi asilia zilizowekwa kimiminika kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
Nchi hizo tatu zimetia saini mikataba kuhusu ripoti ya upembuzi yakinifu na masuala mengine, ikiwa ni pamoja na makubaliano nyeti kati ya makampuni ya nishati ya serikali. Mradi huo umepewa msukumo kutokana na ongezeko la mahitaji ya gesi na kupanda kwa bei ulimwenguni kote kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Commentaires