top of page

NDEGE NYINGINE YAPATA AJALI MAREKANI, 7 WAFARIKI 5 WALAZWA HOSIPITALI


Na VENANCE JOHN


Watu watano wamelazwa hospitalini hapo jana baada ya ndege ya Medevac iliyokuwa imebeba mtoto mgonjwa na mama yake kuanguka katika kitongoji cha makazi huko jimboni Philadelphia ambapo watu saba walifariki dunia.


Watu wote sita waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya Medevac yenye injini mbili walifariki, pamoja na mtu mmoja kwenye gari lililokuwa chini. Meya wa Philadelphia Cherelle Parker amesema kuwa takriban watu 22 waliokuwa chini walijeruhiwa, na kwamba watatu kati yao wako katika hali mbaya. Nyumba 11 za makazi ziliharibiwa kwa kiasi kikubwa na ajali hiyo.


Maafisa bado wanafanya kazi kubaini chanzo cha ajali hiyo, huku wachunguzi wakipata kinasa sauti cha chumba cha marubani hapo jana. Watu 6 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa raia wa Mexico, akiwemo mtoto ambaye alikuwa akitibiwa ugonjwa katika Hospitali ya Watoto ya Shriners iliyoko kaskazini mashariki mwa Philadelphia na mama yake.


Walikuwa wakirudi nyumbani Mexico baada ya matibabu ya msichana huyo na ilitajiwa kuwa ndege hiyo ingetua uwanja wa Tijuana. Ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na Kapteni Alan Montoya Perales mwenye umri wa miaka 46, na rubani mwenza Josue de Jesus Juarez wa miaka 43. Waliandamana na Dk. Raul Meza Arredondo na mhudumu wa afya Rodrigo Lopez Padilla, wote wenye umri wa miaka 41.


Ndege hiyo aina ya Learjet 55 ilikuwa imetoka tu kupaa na ilikuwa ina chini ya dakika moja toka kupaa ilipoanguka katika kitongoji cha makazi, na kuteketeza nyumba tano na magari mengi kwa moto.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page