top of page

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKIA MTONI BAADA YA KUGONGANA NA HELIKOPTA YA KIJESHI MAREKANI

Na VENANCE JOHN


Shirika la usimamizi wa safari za ndege nchini Marekani limesema kuwa ndege ya shirika la ndege la American Airlines imegongana angani na helikopta, eneo la Washington DC. Abiria 60 na wafanyakazi wanne walikuwa kwenye ndege ya America Airlines ambayo imegongana na helikopta karibu na Uwanja wa Ndege wa Kitaifa wa Reagan wa Washington. Ndege hiyo ilikuwa ikitumiwa kwa safari za kibiashara na American Airlines na ilikuwa ikielekea Washington kutoka Kansas.


Afisa wa Jeshi la Marekani amethibitisha kwamba helikopita ya kijeshi ya Black Hawk imehusika katika ajali hiyo. Ajali hiyo imetokea wakati ndege inakaribia kwenye barabara ya uwanja wa ndege wa Kitaifa wa Reagan Washington.


Mamlaka ya usafiri wa anga wa marekani inachunguza chanzo cha ajali hiyo na kulingana na Idara ya zimamoto, ndege hiyo ilianguka katika Mto Potomac. Idara hiyo imesema katika ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba boti za kuzima moto zilikuwa zimefika mtoni kwa ajili ya uokoaji.


Uwanja wa Ndege wa Kitaifa wa Ronald Reagan (DCA) umesimamisha safari zote za ndege huku huduma za dharura zikishughulikia ajali hiyo. "Safari zote za kupaa na kutua zimesitishwa katika uwanja wa ndege wa DCA," mamlaka ya uwanja huo wa ndege ilisema kwenye mtandao wa X.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page