Na VENANCE JOHN
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_5b0875f213704899ba2bd982bcddd5dc~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_5b0875f213704899ba2bd982bcddd5dc~mv2.jpeg)
Jeshi la Zimbabwe (ZDF) limetangaza kuwa rubani kijana mwanafunzi kutoka Kambi ya Jeshi la Wanahewa la Josiah Tungamirai huko Gweru, Mkoani Midlands amefariki katika ajali ya ndege ya mafunzo. Taarifa hiyo imesema ajali hiyo imetokea wakati rubani alipokuwa kwenye mafunzo peke yake.
Ajali hiyo imetokea karibu kilomita 5 mashariki mwa mji wa Guinea Fowl. Hakukuwa na majeruhi ya raia wala uharibifu wa mali. Jeshi la Anga la Zimbabwe limeunda tume ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Comments