Baada ya video kusambaa mtandao zikimuonesha msanii na Mjasiriamali Maarufu Shilole akiwa

na mwanaume mwingine jambo lililoacha maswali mengi ya kwamba je ameachana na mumewe? Hatimaye ukweli umefahamika baada ya mume wa Shilole Bwana Rommy 3D kufunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram
"Habari Ndugu zangu kama ambavyo mmeona kwenye mitandao na hiyo ndio hali halisi basi Mimi na aliyekuwa mwenzangu Zuwena Mohamed (Shilole) Naona tumefikia Mwisho na si Vibaya nikakubali matokeo na kumpisha Kijana mwenzangu aendeleze gurudumu hili, na Maisha yaendelee... nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa vile tulivyoishi siku zote za mapenzi yetu Wabillah Tawfiq"
Comments