top of page

NGUMI ZAPIGWA KATIKA MECHI BAADA YA WIMBO WA TAIFA WA MAREKANI KUZOMEWA NA CANADA

Na VENANCE JOHN


Mashabiki wa Marekani na Canada wametwangana ngumi katika mechi ya hoki ya barafu baada ya wimbo wa taifa wa Marekani kuzomewa. Kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja, mashabiki wa Canada walizomea wimbo wa taifa wa Marekani kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya Marekani katika mashindano ya pande nne ya hoki ya barafu.


Gazeti la New York Post limeripoti kuwa, katika hali ambayo mvutano kati ya Marekani na Canada unaongezeka kufuatia kauli ya Rais Donald Trump kwamba Canada itaunganishwa na Marekani na kulifanya kuwa jimbo la 50 la nchi hiyo, mashabiki wa Canada waliokuwepo uwanjani ambapo timu yao ilikuwa inamenyana na Marekani walipaza sauti kuzomea wimbo wa taifa wa Marekani.


Mapigano hayo yalianza baina ya wachezaji wa timu mbili kabla ya mashabiki zaidi ya 20,000 kuvamia uwanja na kugeuza mechi hiyo kuwa ya masumbwi. Mashindano hayo yanayofanyika nchini Canada yanazikutanisha wenyeji Canada, Marekani, Finland na Sweden.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page