top of page

NIGERIA MAMA WA KAMBO MBARONI KWA TUHUMA ZA KUCHOMA WANAE WA KAMBO MIKONO KISA KULA WALI ALIOHIFADHI KWA AJILI YA BABA YAO....

Maafisa wa polisi wa Jimbo la Adamawa huko nchini Nigeria, wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 23, aliyejulikana kama Rachel Geoffrey, kwa madai ya kuwachoma moto watoto wake wa kambo wenye umri wa miaka 7 na 3.


Msemaji wa Polisi, SP Suleiman Yahaya Nguroje katika taarifa yake Jumamosi, Mei 18, alisema mshukiwa ambaye anaishi huko Federal Housing Estate, alikamatwa Jumatano, Mei 15.

Kulingana na taarifa hiyo, waliokutwa ni kisa hiko ni Genesis Geoffrey" mwenye umri wa miaka 7 na Ijadai Geoffrey mwenye umri wa miaka 3, walikabiliwa na vitendo kadhaa vya kikatili na ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa mama yao wa kambo baada ya kutengana kwa mama yao mzazi na baba yao wanaishi nae kwa sasa.

Kilicho wasikitisha watu wengi zaidi ni tukio la hivi karibuni ambapo mama huyo wa kambo alipopika wali na kumuwekea mume wake ambaye ndiye baba wa watoto hao na kisha kutoka nje, watoto hao waliokua wenye njaa walichukua na kula chakula hicho cha baba yao. Jambo hilo lilimkasirisha, kisha akawafunga mikono kwa leso na kuwafanya washindwe kukimbia nakisha kuwachoma moto mikono yao na kusababisha majeraha mabaya.”

Bado tunazidi kufuatilia habari hiyo na tutakapopata taarifa zaidi tutakujuza, usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page