top of page

NILIMWAMBIA BABA "NILIKOSEA KUCHEZA TANZANIA" KIJANA BADALA YA KUTAFUTA HELA UNANITUKANA

Muendelezo wa Mambo aliyozungumza Mshambuliaji wa klabu ya Pyramids ya Misri Fiston



Mayele ambaye awali alikuwa Yanga SC kwenye mahojiano na Azam TV.

"Unakuta kuna kijana kama Mimi yuko mkoani huko anakuja kutukana kwenye page yangu badala atafute pesa, unaenda kwa mjomba unapewa 10,000 (elfu 10) unalipa nauli unaingia uwanjani bure, unavunja geti baada ya mechi unaongea 'sisi tumelipa nauli yetu, sisi ndio timu yetu hii' nauli yako? Wakati umepewa elfu 10 na Mjomba."

"Baada ya mechi unabakiza elfu 5 (5,000) unaweka bando unaenda instagram kutukana watu, wewe kijana tafuta pesa kama mimi,"

"[Watanzania] wanashambulia familia yangu. Mtoto wangu wa kwanza ilikuwa siku yake ya kuzaliwa, nimempost kwenye 'comment' watu wanaandika 'ushamba ushamba' mpaka baba akanipigia simu kwamba kuna nini? Mbona sasa sio wewe, wanaanza kuingia kwenye familia kwanini? Nikamwambia, mimi nilikosea kuchezea Tanzania." Mchezaji Fiston Mayele.


Yorumlar


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page