top of page

NJIA YA CHINI YA ARDHI YA KISASA YA KUPITISHA MAGENDO KUTOKA MEXICO MPAKA MAREKANI YAGUNDULIWA

Na VENANCE JOHN


Njia ya chini ya ardhi ambayo inapitisha magendo, inayounganisha Ciudad Juarez, Chihuahua nchini Mexico na El Paso, Texas nchini Marekani, imegunduliwa na mamlaka za nchini Marekani.


Njia hiyo ya ardhini ina karibu kilomita 9.6 na inapitisha madawa ya kulevya kutoka Mexico mpaka Marekani ili kukwepa ukaguzi na kukwepa kukamatwa kwa urahisi na mamlaka za Marekani. Pia imekewa na taa, na mfumo wa kuingiza hewa. Maafisa wa Mexico na Marekani wanafanya kazi pamoja kuchunguza, wakisisitiza ushirikiano wa pande mbili dhidi ya magendo.


Ugunduzi huo unaangazia juhudi zinazoendelea za usalama mpakani kabla ya rais Donald Trump hajaingia ofisni rasmi tarehe 20, Januari.Trump ameshaonya juu ya wahamiaji na masuala ya madawa ya kulevya kutoka kwa nchi hiyo jirani ya Mexico.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page