top of page
Radio on air

NOTI YA KIPEKEE DUNIANI KUANZA KUTUMIKA LEO NCHINI JAPAN.....

Japan leo imeanza matumizi ya pesa mpya kwa mara ya kwanza ili kujaribu kupambana na noti bandia.




Noti hiyo inatumia ruwaza zilizochapishwa (printed patterns) kuleta mwonekano wa kipekee ambapo ni picha moja lakini yenye mielekeo au mionekano mitatu tofauti kufuatana na upande au uelekeo wa uono wako.

Noti hiyo imetumia teknolojia ambayo shirika la uchapishaji la Japan linasema ni pesa ya noti ya kwanza ya aina hiyo duniani.

Katika hafla ya uzinduzi wa pesa hiyo waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema noti hiyo ina sura tatu, ambapo sura ya kwanza inaonesha mfumo wa Japan wa ubepari (Japan capitalism), sura ya pili inaonesha kumwezesha mwanamke na sura  ya tatu inaonesha ubunifu wa teknolojia.

Kwa miezi ya karibuni pesa ya Japan (Yen) imekuwa ikishuka thamani dhidi ya dola ya Marekani.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page