top of page

NYANGUMI ANAYEDHANIWA KUIFANYIA UPELELEZI URUSI AFARIKI DUNIA NCHINI NORWAY

NA VENANCE JOHN


Nyangumi ambaye ni jamii ya beluga aliyekuwa anadhaniwa kutumiwa na Urusi kwa shughuli za ujasusi (upelelezi) amepatikana akiwa amekufa katika Pwani ya Norway.


Nyangumi huyo alionekana kwa mara ya kwanza katika maji ya Norway miaka mitano iliyopita, akiwa amefungwa kamera. Nyangumi huyo aliyepewa jina la utani la “Hvaldimir” inasemekana alipewa mafunzo ya kufanya upelelezi (ujasusi) na Urusi.


Mwili wa Hvaldimir umepatikana ukielea karibu na mji wa Risavika, mji ambao uko Kusini Magharibi mwa Norway na Nyangumi huyo amepelekwa bandarini kwa ajili ya uchunguzi. Shirika la ujasusi la ndani la Norway, liliwahi kusema kwamba kuna uwezekano nyangumi huyo amefunzwa na jeshi la Urusi kwani alionekana kuwazoea wanadamu.


Urusi ina historia ya kutoa mafunzo kwa mamalia wa baharini (viumbe wa baharini) kama vile pomboo (dolphin) kwa madhumuni ya kijeshi ingawa hata hivyo Urusi haijawahi kujibu rasmi madai kama Hvaldimir alipewa mafunzo na jeshi lake.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page