Na Ester Madeghe
Uchunguzi mpya umebaini kuwepo kwa "ongezeko kubwa linalotia wasiwasi" la ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu barani Ulaya hasa baada ya utawala wa Israel wa kuanzisha vita vinavyosababisha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wanaodhulumiwa katika Ukanda wa Gaza.

Utafiti huo uliochapishwa hapo jana Alhamisi na Shirika la Umoja wa Ulaya la Haki za Msingi (FRA) uligundua kuwa karibu nusu ya Waislamu barani Ulaya walikabiliwa na ubaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Ripoti ya FRA imeongeza kuwa hali inazidi kuwa mbaya kwa kasi, hasa katika mwaka uliopita huku taharuki zikiongezeka Asia Magharibi, ambapo sasa "ni vigumu zaidi kuwa Muislamu katika Umoja wa Ulaya."
Utafiti huo, ambao ulifanywa kabla ya utawala wa Israel kuanzisha vita vyake vya mauaji ya kimbari huko Gaza zaidi ya mwaka mmoja uliopita mapema Oktoba 2023, ulihusisha zaidi ya nchi kumi za Umoja wa Ulaya ambapo zaidi ya Waislamu 9,600 walihojiwa kati ya Oktoba 2021 na Oktoba 2022.
Ripoti ya FRA imeongeza kuwa waislamu wa barani Ulaya, wanawake na watoto , walilengwa sio tu kwa ajili ya imani yao ya kidini, bali pia rangi ya macho, nywele na ngozi zao, pamoja na sifa zingine za mwili. Waislamu milioni 26 wanaishi katika mataifa mbalimbali yaliyopo ndani ya Umoja wa Ulaya, unaojumuisha zaidi ya asilimia 5 ya wakazi milioni 448 wa nchi za umoja huo.
Comentários