Na Ester Madeghe,
Mamlaka ya Maendeleo ya Kahawa nchini Uganda (UCDA) ni wakala wa serikali iliyopewa jukumu la kukuza na kusimamia ubora wa kahawa katika mfumo mzima wa thamani. Pia ina jukumu la kusaidia utafiti na maendeleo, kukuza uzalishaji, na kuboresha uuzaji wa kahawa ili kuongeza fedha za kigeni na pia mapato ya nchi na malipo kwa wakulima.

"Baadhi ya mashirika yaliundwa wakati uchumi wetu ulipokuwa unasuasua na mishahara kwa watumishi wa umma ilikuwa chini. Leo hii, baadhi ya mashirika haya yamebakia kutofanya kazi na hayana mantiki. Lengo ni kurahisisha majukumu yao kwa ajili ya utumishi wa umma wenye ufanisi zaidi, " Rais Museveni amesema.
Oktoba 24 na 25, 2024 katika majadiliano makali kati ya wabunge wanaotoka mikoa inayolima kahawa na wanaotoka maeneo ambayo zao hilo halilimwi. Katika kura ya zilizopigwa, ilionekana wabunge 159 kuunga mkono kupeleka Muswada kwa Kamati ya Bunge zima ili kuzingatiwa kifungu baada ya kifungu, wakati wabunge 77, huku wabunge kutoka kwa upinzani, kupiga kura dhidi yake.
" UCDA inateka nyara jukumu la serikali la kutoza ushuru, tangu mwanzoni mwa utawala wetu tulifuta ushuru wa mauzo ya kahawa nje ya nchi. Kwa nini? Ni kwa sababu haileti maana kutoza bidhaa zako za nje, sasa UCDA imerudisha hili, hapo labda ndipo sumu ipo," Rais Museveni ameongezea. Mbali na kahawa kumekuwa na hoja ya kupunguza mamlaka zingine tofauti na kuziweka chini ya wizara husika.
"Kwa heri bodi za mamlaka, wasimamizi wakuu, makatibu binafsi, na umati wote. Baada ya kusoma kwa uangalifu, tunaweza kuchukua wakala mmoja kwa usalama na ubora wa vitu vyote vinavyoweza kumeza - vyakula na dawa - au kutenganisha chakula na dawa," Rais Museveni ameongezea.
Rais Museveni amesema kurekebisha mifumo ya mashirika ya serikali kunamaanisha kuondoa uzembe akidai ni lazima vitendo vya ubadhirifu viondolowe katika mchakato wa uzalishaji ili kuongeza maendeleo na kupunguza gharama.
Comments