top of page

PAUL ALEXANDER BINADAMU ALIYEISHI NA MAPAFU YA CHUMA KWA ZAIDI YA MIAKA 70 AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 78..

Paul Alexander, alikabiliwa na changamoto nyingi za kiafya tangu alipozaliwa mwaka 1946. Alexander alikua moja ya waliokumbwa Kwenye mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa wa Polio katika historia ya Marekani ambao ulikua na kesi takribani 58,000 huku wengi wao wakiwa watoto.

Paul Alexander, mwanaume aliyetumia muda wa miaka 70 ndani ya mapafu ya chuma, amefariki Jumatatu Machi 11, 2024 akiwa na umri wa miaka 78. Alilazimika kuishi ndani ya



mashine hiyo yenye uzito wa pauni 600 baada ya kupatwa na Polio akiwa na umri wa miaka sita.

Ilifikia mahala akawa anajulikana kama "Polio Paul" na moja ya madhara aliyopata kutokana na polio ilikua ni pamoja na kupooza kutoka shingo kwenda chini tangu 1952 kutokana na ugonjwa huo, na kumfanya ashindwe kupumua.

Alikimbizwa hospitalini huko Texas baada ya kupata dalili, na akaamka ndani ya mapafu ya umeme.

Licha ya changamoto zake akawa mwanasheria, mwandishi aliyechapishwa, na juu ya yote amekua na msukumo wa ushawishi kwa watu wengi sana kote ulimwenguni.

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page