top of page

"POLENI SANA KWA KIPINDI KIGUMU TUNACHOPITIA" DICKSON JOB

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa nahodha msaidizi wa klabu ya Yanga SC Dickson Job amefunguka haya


"Wananchi, Poleni sana kwa Kipindi kigumu tunachopitia, Nafahamu Maumivu haya yanachagizwa na ukweli kwamba mnaipenda kwa dhati Timu yenu na Mnatuamini sana wachezaji wenu.


Lakini Msisahau Wananchi, Hakuna wakati sisi tunakua Imara kama pale tunapopitia magumu. Nyie mnakumbuka nyakati nyingi tulizozomewa na watu wote Tulisimama tena kwa matumaini na kuishangaza Dunia ya wapenda soka.Wananchi, Tuchane kalenda yenye kumbukumbu zote Mbaya na tuanze upya kwa Kasi na Tamaa ya kuendelea kuwafanya Mjivunie kuwa mashabiki wa Klabu bora zaidi kwenye Taifa Letu.


Daima Mbele, Nyuma Mwiko."

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page