![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_86aeccf25c6d4d31a63d971a4ea1ee41~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_86aeccf25c6d4d31a63d971a4ea1ee41~mv2.jpg)
Na VENANCE JOHN
Idara ya Huduma ya Polisi nchini Kenya imepiga marufuku kufanyika maandamano katikati mwa jiji la Nairobi na viunga vyake.
Taarifa iliyotolea jana Julai, 17, 2024, imekumbusha umma jukumu la idara hiyo katika usalama wa nchi kulingana na Katiba ya Kenya.
Hayo yanajiri huku Kenya ikiendelea kushuhudia maandamano ambayo yalianza tangu mwezi Juni, kupinga Muswada wa Fedha 2024.
Taarifa ya polisi ilieleza nchi hiyo imekuwa ikishuhudia hasara kubwa, watu kujeruhiwa, kupoteza maisha, mali na biashara zimekuwa zikiharibiwa na kwamba polisi wamepokea taarifa kwamba baadhi ya makundi ya kihalifu yanapanga kutumia vibaya maandamano ya siku ya leo Alhamisi, Julai 18, 2024 kutekeleza mashambulizi na uhalifu.
Comments