top of page

PROF. KINDIKI KUAPISHWA LEO KUWA NAIBU RAIS KENYA BAADA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI RUFAA GACHAGUA

Na VENANCE JOHN


Profesa Kithure Kindiki anaapishwa leo rasmi kuwa Naibu Rais mpya, leo tarehe 1, Novemba 2024 katika Hafla ya kuapishwa itakayofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi kuanzia saa 4 asubuhi Taarifa ya gazeti la serikali ilitolewa saa chache tu baada ya Mahakama kuu kuondoa agizo la kuzuiwa kwa Prof. Kindiki kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.


Hili ni pigo kwa Naibu Rais aliyetimuliwa ofisini Rigathi Gachagua baada ya mahakama ya rufaa ya Kenya kukataa kutoa maagizo ya kuizuia Mahakama kuu kuendelea na kesi ya kuondolewa madarakani.


Tarehe 17 Oktoba aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua aliondolewa madarakani na siku iliyofuata Rais Ruto akamteua Profesa Kithuri Kindiki kuchukua wadhifa huo siku inayofuata. Hoja ya kumtimua madarakani Bw Gachagua ilianzishwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse katika Bunge la taifa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page