top of page

PROFESA JAY AMPA UJUMBE MZITO MKEWE KIPENZI

Ikiwa ni siku ya mfanano wa kuzaliwa kwa mke wa msanii mkongwe wa Hip Hop na mbunge wa zamani wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Profesa Jay, huu ndio ujumbe wa mkongwe huyo kwa mkewe


"Leo ni mfanano wa siku muhimu sana ya kuzaliwa kwa The QUEEN OF my HEART @mke_wa_profjize Nakosa maneno sahihi ya kuandika kuhusu wewe, ila nakushukuru sana kwa UPENDO wako wa kipekee kwangu na kuwa Mama bora kabisa wa mwanetu lisa.profjize na kikubwa zaidi ni kunivumilia na kunipambania kwa Hali na mali na kwa uwezo wako wote katika kipindi chote kigumu tulichopitia wakati naumwa sana, Pamoja na maneno na Uzushi mwingi wa WAJA ila uliziba masikio yako kwa Pamba na kuhakikisha kuwa unasimama pamoja na mimi mpaka leo Mwenyezi Mungu ameyajibu machungu na maombi yetu kwa vitendo na kunisimamisha tena nikiwa na afya njema kabisa, ASANTE SANA My best friend, my BAMBI, My GENERAL, My LAAZIZ, INI Mkalia NYONGO, My HALF and the Love of My LIFE, My Beautiful WIFE @mke_wa_profjize


Hakika umetoa funzo kubwa sana kwa wadada wa kisasa kuwa wavumilivu kwa wenza wao hasa wanapopitia mazingira magumu kama niliyopitia mimi, Wewe ni MALKIA wa NGUVU wa muda wote na wa ukweli kabisa na inakupasa uanzishe Chuo cha kuwafunda wadada wa mjini maana halisi ya uvumilivu wakati wa DHIKI na RAHA


HAPPY BIRTHDAY TO YOU MY WIFE Nakutakia maisha marefu zaidi na zaidi yenye mafanikio na furaha tele na tuwe Pamoja mpaka tutembelee MIKONGOJO".

Kheri ya siku ya kuzaliwa @mke_wa_profjize

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page