Na VENANCE JOHN
Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais wa nchi hiyo Joe Biden ameambukizwa virusi vya Covid-
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_c0e5ea3910d541a7adb2e2b672381ab5~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_c0e5ea3910d541a7adb2e2b672381ab5~mv2.jpg)
19 na kwamba ana dalili ambazo sio kali sana.
Mkuu wa vyombo vya habari wa ikulu, Karine Jean-Pierre amesema rais wa Marekani alipewa chanjo pamoja na ile ya nyongeza.
Biden, alipimwa na kukutwa na Covid mara mbili hapo awali.
Bi Jean-Pierre alisema rais alipanga kujitenga nyumbani kwake huko Delaware huku akitekeleza majukumu yake yote kikamilifu.
Daktari wa rais, Kevin O'Connor, amesema Bw Biden alikuwa na dalili za matatizo ya kupumua, ikiwa ni pamoja na mafua na kikohozi na alipewa dozi yake ya kwanza ya Paxlovid.
Biden mwenye umri wa miaka 81, alionekana mapema jana akiwatembelea wafuasi wa chama chake huko Las Vegas na kuzungumza katika hafla iliyokuwa imeandaliwa lakini alifuta hotuba ya kampeni baadaye usiku.
Biden anakabiliwa na shinikizo kubwa la kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais kwa sababu ya umri wake.
Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba Kiongozi wa walio Wengi katika Seneti Chuck Schumer na Kiongozi wa walio Wengi katika Bunge Hakeem Jefferies - Wana -Democrat wawili wakuu katika Bunge la Marekani - walikutana na Bw Biden kwa faragha na nyakati tofauti na kueleza kwamba kuna wasiwasi mkubwa kuwa mgombea wake anaweza kuathiri vibaya ushindani katika Bunge na Seneti.
Comments