Na VENANCE JOHN
Rais wa Rwanda Paul Kagame ametoa onyo kali kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, akisema kwamba Rwanda imejiandaa kwa makabiliano iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo kuzua wasiwasi wa kidiplomais kati ya Rwanda na Afrika Kusini.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_e93b80006ad6483b99b24a416265eaf5~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_e93b80006ad6483b99b24a416265eaf5~mv2.jpeg)
Taarifa ya Rais Kagame ilikuwa inajibu maoni ya Rais Cyril Ramaphosa juu ya jukumu la Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda na Kikundi cha Waasi cha M23 katika mapigano yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Jibu la Rais Paul Kagame kwa Cyril Ramaphosa linaashiria mzozo mbaya wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Rwanda.
Kwa maneno makali Kagame amemjibu moja kwa moja Cyril Ramaphosa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Bwana Kagame alimshtumu Rais wa Afrika Kusini kwa kupotosha mazungumzo ya faragha juu ya hali tete mashariki mwa Congo DRC.
Comments