top of page

RAIS SAMIA AAGIZA MTOTO WA DARASA LA TATU ATENGENEZEWE MGUU BANDIA.

Na VENANCE JOHN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samaia Suluhu Hassan ameagiza viongozi



wanaofanya kazi kwenye ofisi ya rais kwa kushirikiana na wizara ya afya kushughulikia matibabu ya mtoto wa darasa la tatu ya kumwekea mguu wa bandia.

Rais Samia ametoa agizo hilo wakati akiwahutubia wananchi wa Tunduma, mkoani Songwe leo Julai 18, kwenye mkutano wa hadhara.

Mtoto huyo kwa jina la Ebenezer Wile Mwakasyele anasoma shule ya msingi Tunduma mwenye umri wa miaka 8, ana ulemavu wa mguu.

Mtoto huyo alikuwa kando ya barabara akimsikiliza Rais Samia wakati akiwahutubia wananchi.

Rais Samia yuko mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi, baada ya kumalizika kwa ziara ya kikazi mkoa wa Katavi na Rukwa.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page