top of page

RAIS SAMIA ATOA SHILINGI BILIONI 66 KUREJESHA BARABARA ZILIZOHARIBIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni



66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha ili shughuli za usafiri na usafirishaji zisikwame.

Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mohamed Besta amesema fedha za ukarabati wa miundiombinu hiyo zimeshapelekwa mikoa yote nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote ya nchi na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharura vilivyopo Tanroads pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathmini iliyofanyika, mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara kuu za mikoa yote nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini mwa nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinanyesha.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page