Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la uzinduzi wa albamu mpya ya staa wa Bongo Fleva Harmonize
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_ed27344777174e238c7f331f00122394~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_ed27344777174e238c7f331f00122394~mv2.jpg)
Mlimani City Dar es Salaam Jumamosi ya Mei 25.
Kupitia kurasa za mtandao wa Instagram za Harmonize, Efm na Mkurugenzi wa Efm Francis Cizza maarufu kama Majizzo wameweka wazi hilo kwa kuandika ujumbe huu
"Natambua juhudi unazozifanya usiku na mchana kuijenga Tanzania bora, Natambua mchango wa Serikali yako ya awamu ya sita kwenye sekta ya burudani iliyoajiri vijana wengi zaidi.
#FloorNamba Tatu Tupo tayari kukupongeza na kuyasherehekea mengi makubwa unayoyafanya kwaajili yetu. Karibu Dkt Rais Samia Suluhu Hassan (@samia_suluhu_hassan)".
Comments