top of page

RAIS TRUMP ATUMA WANAJESHI 1500 MPAKANI NA MEXICO KUWAZUIA WAHAMIAJI

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani, Donald Trump ameamuru maafisa wa Marekani kuandaa mipango ya kurudisha mara moja wahamiaji wasiokuwa na hati za kisheria kama sehemu ya juhudi za kupambana na kile alichokiita uvamizi kwenye mpaka wa kusinimwa nchi hiyo.


Hatua hii inakuja wakati huo huo Marekani ikituma wanajeshi 1,500 zaidi mpakani na Mexico ili kupanua mchakato wa kufukuza watu wasio na kibali walioingia Marekani haraka. Trump pia amesitisha usafiri na vibali kwa wakimbizi, akisema Marekani haiwezi kubeba idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi.


Uamuzi huu umewaacha maelfu ya watu wakiwa wamekiwa njia panda kwani wanangojea kuingia Marekani. Zaidi ya raia 1,600 wa Afghanistan walikuwa wamethibitishiwa kuingia Marekani, lakini kwa amri ya Trump mipango yao imeingiliwa.


Msemaji wa ikulu ya Marekani,Caroline Leavitt, amesema kwamba Trump anatuma ujumbe mzito sana kwa mataifa yote duniani kwa hatua hizi. Mabadiliko haya ya kuwafukuza wakimbizi yanaweza kupingwa mahakamani, na baadhi ya miongozo ya zamani, kama ile inayozuia maafisa kuingia maeneo ya kimsingi kama shule.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page