Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema atasitisha misaada yote ya kifedha kwa nchi ya Afrika Kusini, kwa kile ambacho amesema mamlaka zinachukua ardhi kwa nguvu na kuzibagua baadhi ya jamii.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_de7e63d985044a0586ac15c6b6df0175~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_de7e63d985044a0586ac15c6b6df0175~mv2.jpeg)
Trump amesema kitendo cha kunyakua ardhi hakikubaliki, akisema ufadhili wote ujao kwa Afrika Kusini utatolewa baada ya kukamilika kwa uchunguzi. Mwezi uliopita, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alitia saini muswada unaoeleza kuwa serikali inaweza, katika hali fulani, kutolipa fidia kwa mali ambayo itanyakuliwa kwa maslahi ya umma.
Trump amependekeza na kuahidi kukata msaada na fedha zote kwa Afrika Kusini, siku kama jibu la kukabiliana na unyakuzi wa ardhi akisema ni unyanyasaji mbaya wa tabaka fulani la watu. Kulingana na takwimu (data) za serikali ya Marekani, nchini hiyo ilitenga karibu dola milioni 440 za msaada kwa Afrika Kusini mwaka 2023.
Suala la ardhi nchini Afrika Kusini limekumbwa na mgawanyiko kwa muda mrefu, huku juhudi za kurekebisha ukosefu wa usawa wa kumiliki ardhi kwa zazungu na Waafrka Kusini zikisababisha ukosoaji kutoka kwa matajiri akiwamo Elon Musk.
Comments