top of page

RAIS WA AFRIKA KUSINI AMPIGIA SIMU ELON MUSK

Na VENANCE JOHN


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amempigia simu Elon Musk kama juhudi za kupunguza wasiwasi wa kutokea mgogoro wa kidiplomosia kati ya Marekani na nchi yake. Hatua hiyo inakuja baada ya Elon Musk kukosoa sheria mpya ya ardhi aliyoisaini Rais Ramaphosa mwezi uliopita huku Rais wa Marekani Donald Trump akitishia kukata misaada ya kifedha kwa Afrika Kusini


Musk ni mshauri wa karibu wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye siku ya Jumapili alitishia kusitisha ufadhili kwa siku zijazo kwa Afrika Kusini kwa madai kuwa nchi hiyo inanyakua ardhi na kuwatendea vibaya watu wa tabaka fulani. Bilionea huyo wa teknolojia mzaliwa wa Afrika Kusini alichapisha ukosoaji wake kupitia wa X, akiuliza kwa nini Ramaphosa ana sheria za wazi za ubaguzi wa rangi katika umiliki wa ardhi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page