top of page

RAIS WA CAF MOTSEPE ASEMA ANADHANI AZIZ KI ALIFUNGA BAO HALALI DHIDI YA MAMELODI.

.Rais wa shirikisho la soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amekiri kuwa goli la Yanga lililokataliwa mwamuzi katika mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini lilikuwa goli halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo leo alipowasili visiwani Zanzibar katika fainali za African



schools football na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa TFF Wallace Karia.

"Nilivyokutana na Rais Wallace baada ya mchezo wa Mamelodi dhidi ya Yanga nilimwambia 'nilidhani lile ni goli' kama Rais wa CAF sikutakiwa kusema chochote lakini mnajua, na napaswa kuheshemu mchakato na taratibu zote, lakini kama shabiki wa mpira nilivyoangalia niliona ni goli halali".

"Lakini tunatakiwa kufuata na kuheshimu sheria na VAR lakini nadhani jambo kubwa ni mashabiki kujiamiani tunawahakikishia kuwa Waamuzi, VAR ni 'WORLD CLASS' na tunahakikisha tumeweka fedha nyingi," Rais wa Shirikisho la Mpira Afrika (CAF), Patrice Motsepe. Ikumbukwe kuwa Goli hilo lilifungwa na kiungo wa Yanga Stephen Aziz Ki ambapo mwamuzalilikataa kwa kile alichoamini mpira haukuvuka mstari wa goli.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page