top of page
Radio on air

RAIS WA IRAN AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA HELIKOPTA..

Taarifa zilizotufikia mezani zinaeleza kuwa Rais wa Iran Ebrahim Rais amefariki Dunia pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian na Viongozi wengine ambao walikuwa wakisafiri pamoja kwenye Helikopta ambayo imeanguka Kaskazini Magharibi mwa Iran wakati Rais huyo na Timu yake wakitokea kwenye shughuli ya kikazi mpakani mwa Nchi hiyo na Azerbaijan ambapo hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo.


Chombo cha Habari cha Serikali ya Iran kiitwacho IRNA kimethibitisha vifo hivyo na kusema tayari Baraza la Mawaziri la Serikali ya Nchi hiyo limekutana kwa dharura, AFP na Reuters wamethibitisha pia vifo hivyo.

Taarifa za vifo hivyo zimethibitishwa baada ya zoezi la kuisaka ilipoangukia Helikopta hiyo kufanyika kwa saa kadhaa hadi usiku wa kuamkia leo na baadaye mabaki ya Helikopta yamepatikana katika mazingira ambayo yameashiria hakuna aliyepona katika ajali.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin alituma Ndege mbili za uokoaji pamoja na Waokoaji 50 kusaidia uokoaji ilipoangukia Helikopta hiyo usiku wa kuamkia leo huku akiahidi pia kuisaidia Iran kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo ambayo inajiri huku kukiwa na mzozo mkali kati ya Iran na Israel na kupelekea baadhi ya Watu kuhusisha ajali hiyo na mzozo huo ingawa taarifa za awali kutoka Iran zinadai chanzo cha ajali ni mabadiliko ya hali ya hewa angani.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page