Taarifa zilizotufikia mezani Rais wa Kwanza wa nchi ya Namibia, Sam Nujoma amefariki Dunia akiwa na umri wa Miaka 95.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_d6c34d3ab57b4bddb039037c2af148f6~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_d6c34d3ab57b4bddb039037c2af148f6~mv2.jpeg)
Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Afrika Kusini Mwaka 1990 ilipopata Uhuru. Moja ya matukio yake ya kukumbukwa ni Mwaka 1960 alipokimbilia Nchini Tanzania kutokana na vuguvugu lililotokea Namibia, ambapo Hayati Mwalimu, Julius alimpatia hifadhi
Baada ya Uhuru alichaguliwa kuwa Rais na kudumu hadi Mwaka 2005 ambapo aliamua kustaafu ila alibaki kuongoza Chama cha South West Africa People's Organisation (SWAPO) hadi Mwaka 2007.
Comentarios