![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_ce2e0c037f6448f9b725cb6d5ea54669~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_ce2e0c037f6448f9b725cb6d5ea54669~mv2.jpeg)
Rais wa Yanga SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng. Hersi Ally Said @caamil_88 ameshinda Tuzo ya Mwanamichezo mwenye mchango kwenye maendeleo ya Mpira wa Miguu Barani Afrika.
Sherehe za tuzo hiyo ya Nigeria-France Sports Awards, zilifanyika mwanzoni mwa juma jijini Paris, Ufaransa. Tuzo hiyo ilipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Ali Jabir Mwadini.
Comments